SAKATA LA URAIS ACT KITENDAWILI, MPINA KIKAANGONI TENA.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Monalisa Ndala amepinga uamuzi wa chama hicho, kumteua Luhaga Mpina kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, akidai amekosa sifa.

Kada huyo amedai kanuni za chama hicho, zimekiukwa katika uteuzi wa Mpina, kinyume na taratibu na sheria ya uchaguzi inayoelekeza mtia nia anayependekezwa na chama cha siasa, kukidhi taratibu za kimchakato za ndani za chama husika.

Kutokana na hilo, jana terehe 14 Monalisa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu akimtaarifu kwamba Mpina hajakidhi kanuni za kudumu za uendeshaji wa hicho, toleo la mwaka 2015.

Katika barua hiyo, Monalisa amesema vipengele kadhaa vya kanuni namba 16 inayozungumzia sifa za mgombea ndani ya chama na wanaomba kuteuliwa kugombea ACT Wazalendo, vimekiukwa.

Akinukuu vipengele hivyo, Monalisa amesema,“Kanuni namba 16(4) mgombea urais / viongozi wa chama ngazi ya Taifa, lazima awe mwanachama wa ACT Wazalendo kwa muda usiopungua mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mwisho ya uteuzi ya mgombea wa chama,”

Ameongeza kuwa, “Mgombea wetu aliyejiunga siku mbili kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais baada ya kuenguliwa kuwania ubunge kwa chama chake cha zamani [CCM] Julai 28, 2025,” ameeleza Monalisa ambaye ni mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Monalisa ameendelea kusema kuwa Mpina amepingana na kanuni namba16 (4) (iii) inayosema awe tayari kutangaza mali binafsi na vyanzo binafsi kabla ya kuteuliwa kugombea kwa kufuata utaratibu ulioanishwa sehemu ya (vii) ya nyongeza ya Katiba ya ACT Wazalendo.

“Kwa bahati mbaya au makusudi mgombea wetu amevunja kanuni hii kwa kuwa hadi anatangazwa kuteuliwa kuwa mgombea, hakuna pahala popote ameonyesha kutangaza mali zake,” amefafanua Monalisa katika barua hiyo ambayo nakala imeenda Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Katika barua hiyo, Monalisa amedai kuwa Mpina amekiuka kanuni muhimu namba 16 (4) (iv)inayomuhitaji kuelewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT Wazalendo kama inayosomea ‘awe ni mtu aliyethibitika kuielewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT Wazalendo

0 Maoni