NI ZAIDI YA USHINDI BABATI, KHAMBAY ACHUKUA FOMU

Mgombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Babati Mjini, Emmanuel Khambay, leo Agosti 26, 2025, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Halmashauri ya Mji wa Babati akiambatana na mkewe.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Khambay ameahidi kushirikiana na serikali kuendeleza jitihada za kusukuma maendeleo ya jimbo hilo, huku akiwataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa kura ya maoni ili kujenga mshikamano wa pamoja utakaokiwezesha chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

“Mshikamano wetu ndani ya chama ndiyo silaha ya ushindi, ni wakati wa kuungana kwa pamoja kuhakikisha CCM inaendelea kuaminiwa na wananchi wa Babati Mjini,” alisema Khambay.

Mamia ya wakazi wa mji huo pamoja na wafanyabiashara wakubwa walijitokeza kumsindikiza mgombea huyo hadi alipochukua fomu, wakionesha hamasa kubwa ya kisiasa.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wagombea ubunge na udiwani wanatakiwa kurejesha fomu zao kabla ya kesho Agosti 27, 2025 saa 10 jioni, huku kampeni zikitarajiwa kuanza rasmi Agosti 28, 2025.





0 Maoni