MAFUNZO ULINZI WA AMANI UHIMARISHA UELEWA NA USHIRIKIANO

Na. Sgt. Geofrey Jacka - DODOMA

Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Mhandisi Bonanza Malata, leo Julai 16, 2025 amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP. Jeremiah Katungu, kwa kutoa fursa kwa Maafisa na Askari, kushiriki katika mafunzo mbalimbali ya Ndani na nje ya Nchi, ikiwemo ya ulinzi wa amani ambayo yame endelea kuimarisha uelewa na ushirikiano.

SSP. Malata ameyasema hayo siku chache baada ya kurejea Nchini akitokea Afrika Kusini, alipokuwa akipata mafunzo ya ulinzi wa amani katika Chuo cha Taifa cha Vita cha Nchini humo (South Africa National War College - SANWC), kuanzia Juni 22 - 26, 2025 ambapo Maafisa kutoka Nchi Nane za SADC walishariki.

Aidha SSP. Malata ambaye amewahi kushiriki katika misheni ya ulinzi wa amani Nchini Kongo ameshauri kuwa, mafunzo hayo yawe endelevu kutokana na umuhimu wake na kushirikisha Maafisa wengi zaidi, ili Jeshi na Taifa liweze kunufaika pindi kunapotokea uhitaji wa Maafisa na Askari kwenda kwenye misheni za Ulinzi wa amani.


0 Maoni