Wakusanya Ushuru Wa Maegesho Mkoa Wa Dar Es Salaam Wafundwa

 Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) jana tarehe 28 Novemba, 2021 imeendesha Semina ya kuwajengea uwezo Wakusanyaji Ushuru wa Maegesho wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya matumizi ya mfumo wa Kielektroniki wa Ushuru wa Maegesho (TeRMIS).

Na. Mwandishi Wetu

Wakusanyaji Ushuru  wameelimishwa kuwa na lugha nzuri ya kuwahudumia wateja wa maegesho pale wanapotumia maegesho (customer care). Pia wameelimishwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuongeza tija na ufanisi katika kutimiza majukumu yao.

Wakusanyaji Ushuru wamehimizwa kuwaelimisha wateja pale wanapotoa huduma ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima.

Mfumo wa maegesho Kidigitali unatarajia kuanza kutumika kuanzia 1 Desemba, 2021 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Singida na Dodoma.



1 Maoni