Mkurugenzi wa Tambaza Auction mart & General Broker Bw.Abdalla.H.uweje,Ameilalamikia serikali upande wa wizara ya fedha kupiga mnada kwa kusimamiwa na katibu mkuu wa wizara hiyo na wao kukosa kazi.
akizungumza na blog hii amesema wizara hiyo imekua ikipiga mnada mara kwa mara badala ya kuwapa tenda makampuni yaliyopewa leseni kwa ajili ya minada ya mahakama,kitu ambacho kinasababisha makampuni yao kukosa kazi huku wakiendelea kulipa kodi.
Akaendelea kusema kua katika kumbukumbu ya gazeti la Mtanzania la ijumaa feb.11/2011 wizara hiyo
ilipiga mnada ya vitu mbali mabali yakiwepo magari ya aina mbali mbali kama Isuzu Troper,Prado,Hilax,Hice,Benzi na mengine zaidi ya ishirini ambayo yalipigwa mnada jijini Dar es salaam.
"Mimi nashangaa sana katibu mkuu wa wizara anaruhusu mnada ufanyike na wizara wakati makampuni wamewapa leseni kwa ajili ya kupiga minada hiyo na vile vile wao hawna uzoefu na shughuli za mnada , alisema bwana Uweje.
0 Maoni