Mkurugenzi wa benki ya wanawake Tanzania Women'S Bank Ltd Bi. Margareth Mattaba Chacha ametoa wito kwa wanawake na makampuni kununua hisa, au kufungua akaunti ili kuboresha uchumi wao wenyewe.
Akizungumza ofisini kwake na Nccomediatz.blog jijini Dar es salaam Bi. Chacha amesema Benki hiyo imekuwa ikiwanufaisha wakinamama kwa kuwapa mikopo kwa riba nafuu ambapo mpaka sasa zaid ya wanawake 600,000 wamepata mafanikio.
"Hapa kwetu tunatoa mikopo kwa riba nafuu sana, kwa mfano mtu akichukua 200,000 kwa miezi sita anarudisha 225,000 na akaunti zetu ni Shs/=3000 tu bila usumbufu, hivyo basi wakinamama waje kuwekeza ili nano waweze kuwa na hisa kubwa na badaye wanaweza kuchukua mikopo kiurahisi zaidi tofaut na sasa serikali ndiyo ina hisa kubwa,'ailisema Bi. Chacha.
Hata hivya amesema wakinamama ndio waliyoomba Benki ya wanawake ifunguliwe na baadaye 1999 ikafunguliwa na Raisi Jakaya kikwete na sasa serikali ina hisa ya asilimia 97. Alisema kwa sasa wako katika mipango ya kuengeza matwi mengine na vilevle wanatarajia kuwasaidia vijana wa kike wanaomaliza vyoo na kukaa nyumbani kwa kuwapa mikopo.
0 Maoni